Habari Mseto

Mwanamke auawa na umati akidaiwa kuwa mchawi

October 27th, 2020 1 min read

RUTH MBULA NA FAUSTINE NGILA

Mwanamke wa miaka 70 aliuwawa na wanakijiji waliokuwa wamejawa na ghadhabu kwenye kjiji cha Nyabitiro Kaunti ya Kisii kwa madai kwamba alikuwa mchawi.

Mwanamke huyo alivamiwa Jumanne asubuhi baada ya kuripotiwa kuwa alipatikana akiangusha gusha majani yanayoaminika kuwa ya kichwani nyumbani kwa mwanawe wa kambo.

Wanankijiji walisema kwamba mwananwe alikuwa amezika mwananwe wa kike wa miaka sita wiki iliyopita .Wlidai kwamba huyu ndiye mtoto wa tatu ambaye aliyepoteza kwa njia zizizoelekweka..

“Tumepotetza Watoto watatu kwa njia amabazo hazijulikani tangu tuoane mwaka 1997,”alisema mwanaume huyo..

Msichana aliyefariki hivi majuzi alipata mafua na akakfariki punde tu alipofikishwa hospitalini.

Wakazi walisema kwamba walipomvamia mwanamke huyo alitaja majirani wawili ambao walihusika naye kwenyevitendo vya uchawi.

Lakini wawili hao walifanikiwa kutoroka kabla ya umati uliojawa na ghathabu kuwapata .Nyumba zao zilivamiwa na kuchomwa.Mwanawe ambaye anafanyakazi kama bawabu alisema kwamba mwanamke huyo aliikuwa ameonywa na wanakijiji na hakusikia.

Taifa Leo haikuweza kupata thibitisho ya madai hayo ya uchawi.