Habari Mseto

Mwanamke azuiliwa kwa utekaji nyara

November 9th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Polisi Naivasha wanamzuilia mwnamke mmoja wa mika 35 kwa madai ya kuteka nyara lori moja, tukio lililotokea mapema Jumatano asubuhi.

Polisi walisema kwamba  mwanamke huyo alikuwa na watu wengine watatu walioteka nyara Lorieneo ya Eldama Ravine ,Baringo na kuwapeleka wawili hao waliotekwa nyaraa wakiwa hawajisikkii maeneo ya Naivasha.

 Kamanda wa polisi waKaunti Ndogo ya Naivasha Sameul Waweruakisimulia kisa hicho alisema kwamba polisi waliokuwa wakifanya Patrol walaiona lori hilo maeneo ya Kasarani kando ya barabara ya kuu ya Naivasha-Gilgil

 “Maafisa hao walisimamisha lori hilo lakini waliokuwa ndani yake hawakulisimamisha huku wakilazimisha kuliendesha kwa kasi ,”Bw Waweru aliambia Taifa Leo.

 Maafisa hao walikamata washukiwa hao waliokuwa wakitorokea eneo ya Eburu ambapo waliacha gari hilo.

“Polisi walipochunguza walipata watu wawili waliokuwa hawajitambui ndani ya lori hilo kwenye kiti cha nyuma,”alisema Bw Waweru.

Polisi walisema mshukiwa huyo anasaidia polisi kwenye uchunguzi.Alisema kwamba waathiriwa wapokea matibabu na wanendelea vizurikwenye hospitali ya Naivasha.

 “Tunagoja wapate fahamu ili waandikishe taarifa,”alisema Bw Waweru.

 Maafisa wanao chunguza kisa hicho lori hilo limekuwa likitekwa nyara mara kwa mara.

 “Kukamatwa kwa washukiwa hao ni njia moja ya kupigana na utekjai nyara,”alisema mkuu huyo wa polisi Naivasha.