Kimataifa

Mwanamke kortini kwa mazoea ya kushiriki ngono na maiti

July 15th, 2019 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU

MWANAMKE mfanyakazi wa mochari moja Marekani alikamatwa, baada ya kubainika kuwa mtoto ambaye alijifungua majuzi alitokana na kufanya ngono na mwanamume maiti, ambaye alikuwa amepewa kazi ya kumfanyia upasuaji.

Jennifer Burrows ambaye alikuwa msaidizi wa daktari wa upasuaji anatuhumiwa kuwa amekuwa akifanya ngono na wanaume maiti wanapopelekwa mochari kwa miaka miwili sasa, katika kisa husika ikidaiwa alipata uja uzito na akajifungua mtoto mvulana Januari 2019.

Kulingana na idara ya polisi eneo la Kansas, mwanawe Burrows ni mtoto wa mwanamume ambaye aliaga dunia katika ajali ya barabarani mnamo Machi 2017, ambaye Burrows alipewa mwili wake kuufanyia upasuaji.

Burrows anadaiwa kuwa amekuwa akidhulumu maiti za wanaume kingono, hadi sasa idadi ya wanaume maiti aliolala nao ikikisiwa kuwa zaidi ya 60.

Mwanamke huyo anasemekana amekuwa akilala na mili ya wanaume wa kati ya miaka 17 na 71.

“Tulianzisha uchunguzi kuhusu kisa hiki Oktoba, baada ya kufahamishwa kuwa huenda mshukiwa alikuwa akidhulumu maiti kingono,” mkuu wa polisi akaambia wanahabari.

“Kwa miezi michache iliyopita, tulikusanya ushahidi wa kutosha, kuthibitisha kuwa mtoto aliyezaliwa ni wa marehemu. Tulithibitisha kuwa mtoto huyo ni wa mwanamume wa miaka 57 aliyeaga katika ajali ya barabarani Texas. Ushahidi wetu ulionyesha kuwa marehemu hakuwahi kukutana na Burrows kabla ya kifo chake na kuwa mtoto alipozaliwa tayari alikuwa amekufa,” akasema afisa huyo.

Burrows anakumbana na jumla ya mashtaka 158, yakiwamo kutumia maiti vibaya, tabia za aibu na kumiliki dawa haramu.