Habari Mseto

Mwanamke motoni kwa kumuua mumewe na kutupa mwili kwa choo

October 1st, 2020 1 min read

 Na Charles Wanyoro

Polisi Kaunti ya Meru wanamzuilia mwanamke mmoja wa miaka 40 kwa madai kwamba alimuua mume wake na kumzika ndani ya choo akisaidiwa na mwanawe wa kike na kiume.

Mwili wa Julius Kalawa Mikiigu ambao ulikuwa tayari umeanza kuoza ulitolewa kutoka kwa choo na wapelelezi mwezi mmoja baada ya kupotea kijijini Manthi.

Polisi walikamata Margaret Karimi pamoja na mwanawe wa kiume Andrew Mutuma wa miaka 19 na mwanawe wa kike Esther Kawira wa mika 15 wanaoaminika kuhusika na kifo cha Bw Kalawa.

Naibu wa mkuu wa polisi Tigania Magharibi Joel Chepkwony alisema familia hiyo ilikuwa imeripoti kwamba mwathiriwa alikuwa amepotea Agosti 27.

Wakazi waaliambia Taifa Leo kwamba mwathiriwa alikuwa na mzozo wa shamba na wanawe 12.

“Kuna mahala alikuwa ameonyesha mwanawe mahali ajenge nyumba lakini akabadilisha na kumwambia ajenge choo badala ya nyumba mwanawe alikasirika na hapo do mzozo uliaanza ,” alisema Joshua Thuranira.

Mkuu wa polisi alisema kwamba washukiwa hao watafikishwa kortini Jumatano.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA