Kimataifa

Mwanamke mwenye fikra chafu hatarini kusukumwa jela

January 31st, 2019 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU

MAMA mmoja kutoka Glasgow, Scotland yuko kwenye hatari ya kufungwa gerezani, baada ya kujaribu kufanya ngono na mwanaume wa umri mdogo kumliko aliyekuwa usingizini.

Bi Elizabeth Barr wa miaka 40 anadaiwa kumrukia mwanaume huyo wa miaka 27 alipokuwa amelala kitandani katika jumba moja mnamo Septemba 2016.

Korti ilifahamishwa kuwa kisa hicho kilimwacha mwanaume huyo kwa machozi, huku mwanamke huyo naye akidai kuwa walikuwa wameelewana na kuongeza kuwa mwanaume huyo alikuwa na woga kwa kuwa alikuwa na mpenzi.

Lakini mama huyo wa watoto wawili alipatikana na hatia na mahakama moja huko Glasgow. Korti ilimpata na hatia ya kujaribu kufanya ngono na mwanaume aliyekuwa usingizini, ambaye hangeweza kukubali kwa hali hiyo.

Korti ilifahamishwa kuwa Bi Barr alikuwa amekutana na mwanaume huyo saa chache tu kabla ya kisa hicho.

Shahidi mmoja alieleza korti kuwa baada ya kisa hicho, mwanaume huyo alifika katika mlango wa chumba alimokuwa amelala akilia.

Baadaye, polisi walijulishwa na mwanamke huyo akakamatwa.

Lakini Bi Barr alisisitiza kuwa ni mwanaume huyo aliyeanza vitendo vya mapenzi. “Alikuwa akishtuka kuwa mpenzi wake angejua kuwa alikula uroda,” akasema mama huyo.

Mwanamke huyo sasa anatarajiwa kutolewa hukumu baada ya korti kupokea ripoti kutoka idara ya makossa ya kingono.