Habari Mseto

Mwanamke taabani kwa kumuua mpenziwe

November 13th, 2020 1 min read

JOSEPH OPEDA NA FAUSTINE NGILA

Mwanamke wa miaka 21 aliyedaiwa  kumuua mpenziwe  alishtakiwa kwa makosa ya mauaji.

Branswet Wambui Muchiri aliyefika mbele ya jaji  Hillary Chemitei alishtakiwa kwa mauaji ya John Mwangi chumbani walichokodisha  mtaa wa Bismaark Kaunti ya Nakuru Oktoba 21.

Mashtaka yalisema kwamba alimdunga mwezake shingoni kwa kutumia kisu. Bi Wambui alikataa mashtaka hayo na kuomba korti umwachilie kwa dhamana.

Kupitia kwa mwanasheria wake Kairu Maina alidhibitisha kwamba hatoingililia Ushahidi na kushemi tarehe ya korti.

Jaji  Chemitei alimwachilia kwa dhamana yaSh  800,000 ama  dhamana ya feedha yaSh 300,000.

Mshukiwa huyo anaaminika kuwa walizozana na mpeziwe kabla ya kuchukua kisu na akamdunga mara kadhaa.

Awali alikuwa ameandikisha ripoti kwamba Bw Mwangi alifariki kwa kujitia kitazi na kwamba yeye na wezake hawakufika kwa wakati kumuokoa.

Baada ya kufanyiwa upasuaji ulionyesha kwamba Bw Mwangi alifariki kwasababu ya kuvunja damu.

Kwenye eneo la tukio polisi walipata kisu ambayo inaaminika kuwa ndio ilitumiwa kwenye mauaji.

Mshukiwa alishtakiwa baada ya kufanyiwa vipimo vya kiakili.Kesi hio itatajwa tena Februari 8.