Mwanamume afa akiramba uroda lojing’i

Mwanamume afa akiramba uroda lojing’i

Na CHARLES WANYORO 

POLISI katika eneo la Maua, Igembe Kusini, Kaunti ya Meru wanachunguza kisa ambapo mfanyabiashara alipatikana amefia ndani ya lojing’i aliyokodisha kumumunya urojo na wanawake wawili usiku kucha.

Mfanyabiashara huyo aliyetambuliwa kwa jina Kirimi Nkunja anayetoka Muringene, Igembe ya kati aliwasili katika  lojing ya New Ben Bella Jumapili jioni akiandamana na wanawake wawili na kukodisha chumba.

Mnamo Jumatatu watu walishangaa kupata mwili wa mfanyabiashara huyo umefunikwa na shuka kitandani ukiwa uchi. Wanawake aliokuwa nao walitoroka baada ya kuona mpenzi wao ameaga.

Taifa Leo Dijitali ilipozuru eno la mkasa, gari la mwanamume huyo aina ya Toyota Probox lilikuwa limeegeshwa nje ya lojing’i hiyo.

Mamia ya wakazi wa mji huo pamoja na watu wa familia ya marehemu walikusanyika nje ya lojing kuutazama mwili ukiondolewa kupelekwa mochari katika hospitali ya Nyambene kufanyiwa upasuaji.

Shahidi mmoja alisema kondomu nyingi zilikuwa zimetapakaa kote chumbani katika hoteli hiyo ya New Ben Bella.

“Kondomu nyingi zilikuwa mle chumbani. Polisi walifunika mwili wake na blanketi kisha kuutoa kupeleka mochari. Ni aibu mtu kufa katika hali hiyo.Nawahimiza wanaume wawe waaminifu kwa wake zao,” alisema mwendesha boda boda aliyemfahamu mwenda zake.

Rafikiye mhasiriwa huyo alisema huenda alitumia dawa za kuongeza nguvu.

TAFSIRI: WANGU KANURI

You can share this post!

Afueni kwa shule 6 kufunguliwa baada ya miaka saba

Raila atetea kuzungushwa kwa urais