Mwanamume ashtakiwa kudai kwa fujo

Mwanamume ashtakiwa kudai kwa fujo

NA RICHARD MUNGUTI

MWANAMUME aliyetisha kumdunga kisu mchuuzi aliyekuwa anamdai ameshtakiwa.

Simon Omuse alikana mbele ya hakimu mkazi Monica Morara kwamba alizua vurugu na kuhatarisha amani.

Omuse alishtakiwa mnamo Mei 31, 2022 alimtisha Remi Nitanga kwa kisu.

Wakati wa tukio hilo Omuse aliingia kama farasi wa Ngong katika makazi ya mlalamishi na kumdai kwa fujo.

Mlalamishi alipoona maji yamezidi unga alipiga kamsa ndipo akaokolewa na maafisa wa polisi wa utawala.

Polisi walimpokonya Omuse kisu kisha wakamfungulia mashtaka, hakimu alifahamishwa.

Mshtakiwa aliomba korti imwachilie kwa dhamana.

Bi Morara alimwamuru mshtakiwa alipe dhamana ya pesa tasilimu Sh10,000.

Kesi imeorodheshwa kusikilizwa Julai 7, 2022.

Upande wa mashtaka uliangizwa umkabidhi mshtakiwa nakala za mashahidi aandae tetezi zake.

  • Tags

You can share this post!

DOMO: Bahati asiye na bahati!

Mgombea udiwani ashtakiwa kwa kumwandalia mzee safari ya...

T L