Habari Mseto

Mwanamume atozwa faini kwa kushiriki ngono hadharani

May 29th, 2019 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MWANAMUME aliyekamatwa akifanya tendo la kuonana kimwili na mpenziwe wa kike katika bustani ya Uhuru Park alitozwa faini ya Sh1,500 ama atumikie kifungo cha mwezi mmoja gerezani.

Mwanamume huyo alikiri kushiriki ngono mahala pa umma aliposhtakiwa mbele ya hakimu mkuu katika mahakama ya Citi Bi Roselyen Onganyo.

Aliposomewa shtaka alikiri alishiriki ngono na rafikiye huyo wa kike.

Wawili hao walitiwa nguvuni na askari wa jiji la Nairobi na kushtakiwa kwa kukaidi sheria za kaunti ya jiji la Nairobi.

“Naomba hii mahakama inisamehe,” mwanamume huyo alijitetea na kuapa mbele ya mahakama “sitarudia kitendo hiki cha aibu tena.”

Bi Onganyo alimwonya vikali na kumwambia, “Ukirudishwa hapa siku nyingine utaadhibiwa vikali.”

Askari wa jiji walipowakamata wawili hao waliwaachilia kwa dhamana ys Sh500.

Mwanadada hakufika mahakamani kujibu shtaka na hakimu alielezwa “anasakwa kwa vile alikaidi amri afike kortini Jumatano kujibu shtaka.”