Habari Mseto

Mwanamume avua nguo kupinga mkewe kupokonywa kiti

July 4th, 2020 1 min read

COLLINS OMULO na FAUSTINE NGILA

Kulishuhudiwa kizaazaa nje ya bunge la Kaunti ya Nairobi mwanamume alipotoa nguo baada ya kupata habari kwamba mpinzani wa mkewe alikuwa aapishwe kuwa mwakilishi wa kaunti.

Mwanamume anayejulikana kama Job Odour alizua kizaazaa baada ya kujua kwamba Perpetua Mponjiwa alikuwa aapishwe kuchukua nafasi ya mkewe,  Eve Maleya chama cha ODM kilipoteua madiwani.

“Hamuwezi kutoa mke wangu kutoka kwa uongozi. Nataka mrudishe mke wangu kwa kiti,” mwanaume huyo alisikia akipiga mayowe akijaribu kuingia kwenye bunge ya kaunti ya Nairobi.

Kizaazaa hicho kilisababisha msongamano wa magari huku madereva wakiduwazwa na mwanamume huyo.

Diwani wa Mathare Kaskazini Jared Okode anayejulikana kama Defao alilazimika kumbebeleza Bw Odour avae nguo zake.

Bi Malenya aliolewa kwenye orodha ya madiwa wateuliwa na tume ya uchanguzi mwaka jana kufuatia kesi iliyowasilishwa na Bi Ms Malenya.

Alikuwa ampiga kutolewa kwake na kwenda kortini kusimamishwa kuapishwa kwa Bi Mponjiwa.

Bi Malenya alisema anafaa kuteuliwa huku akiomba korti itupilie mbali kuapishwa kwa Bi Mponjiwa.

Alisema Bi Mponjiwa aligombea kiti bila chama chochote mwaka 2017 na hakufaa kuteuliwa kama diwani.