Habari Mseto

Mwanamume avua nguo na kujitia kitanzi baada ya kugombana na mkewe

April 17th, 2024 1 min read

Na FLORAH KOECH

WAKAZI wa kijiji cha Chemogoch, Eldama Ravine, Kaunti ya Baringo wameshangazwa na kisa cha mwanaume mmoja aliyevua nguo zote kabla ya kujitia kitanzi katika shamba lake baada ya kugombana na mkewe.

Kulingana na maafisa wa usalama na chifu wa eneo hilo, Patrick Rono, 34, baba ya watoto watatu alifika nyumbani kutoka sokoni na kupata mkewe ametoroka kitendo ambacho inashukiwa kilimfanya kujiua.