Mwanamume azuiliwa kujeruhi polisi kwa jiwe wakati wa kafyu

Mwanamume azuiliwa kujeruhi polisi kwa jiwe wakati wa kafyu

Na JOSEPH NDUNDA

MWANAMUME anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Makongeni, Nairobi kwa kumgonga afisa wa polisi kwa jiwe na kumjeruhi kichwani.

John Kimwaki Wahu alidaiwa kumpiga konstebo Peter Kamau wa kituo cha polisi cha Makongeni.

Afisa huyo alijeruhiwa akiwa kwa doria karibu na mtaa wa nyumba za Benki Kuu , barabara ya Likoni kuhakikisha kaununi za kafyu zinazingatiwa.

Mwathiriwa alipelekwa hospitalini huku Wahu akikamatwa mara moja.

Afisa huyo bado amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi, hospitali ya Metropolitan, mtaa wa Buruburu.

Mshukiwa huyo sasa anatarajiwa kushtakiwa kwa jaribio la mauaji au mauaji, shtaka likitegemea hali ya afisa huyo.

Inspekta Edward Nzaka alipata maagizo mbele ya Hakimu Mkuu, Bi Emily Ominde wa mahakama ya Makadara kumzuilia mshukiwa kwa siku nne wakisubiri uchunguzi ukamilike.

Bw Nzaka alisema anahitaji muda zaidi kuweza kuandikisha taarifa za mashahidi.

You can share this post!

Afueni adimu kufuatia mafuta kushuka bei

Majaji watatu washinda kesi ya kususia kazi

adminleo