Habari

Mwanasiasa Joe Nyagah afariki akiwa na umri wa miaka 72

December 11th, 2020 1 min read

Na MWANDISHI WETU

MWANASIASA Joe Nyagah amefariki katika Nairobi Hospital Ijumaa akiwa na umri wa miaka 72, ndugu yake Norman Nyagah amethibitishia Taifa Leo.

Joe aliwahi kuhudumu katika baraza la mawaziri la serikali ya Rais wa Pili marehemu Daniel arap Moi ambapo alikuwa Waziri wa Vyama vya Ushirika na Maendeleo.

Alikuwa mwanawe marehemu Jeremiah Nyagah, aliyekuwa mmoja wa mawaziri katika baraza la mawaziri la kwanza la Rais Moi.

Mwaka 2017 Joe Nyagah aliwania urais akiwa mgombea wa kujitegemea.