Habari Mseto

Mwanawe Kajembe azikwa

August 20th, 2020 1 min read

MOHAMED AHMED NA FAUSTINE NGILA

BI Langoni Kajembe, mwanawe wa kike mbunge wa zamani wa Changamwe Ramathan Kajembe amezikwa Alhamisi Mombasa kwenye makaburi ya Shee Mikindani.

Bi Langoni alifariki wiki mbili baada ya mazishi ya babake Bw Kajembe, aliyekuwa mwanasiasa mkongwe wa Pwani.

Alilazwa hospitalini baada ya kuzirai aliposikia habari za kifo cha babake Agosti 7.

“Tangu apate habari za kifo cha babake alianguka na kulazwa hospitalini siku hiyo. Hakupata nafasi ya kuhudhuria mazishi ya babake. Kwa bahati baya, kifo kikamtembelea Jumatano,” rafiki wa familia aliyezungumza na Taifa Leo alisema.

Langoni ni kifunguamimba wa kike na alisemekana kuwa na uhusiano wa karibu sana na baba yake ambaye aliipa mojawapo ya kampuni zake jina la mwanawe.