Habari Mseto

Mwanawe Trump apatikana na corona

July 5th, 2020 1 min read

AFP na FAUSTINE NGILA

Mpenziwe mwanawe Rais wa Marekani Donald Trump amethibitisha kuwa na virusi vya corona, vimeripoti vyombo vya habari nchini humo Ijumaa.

Kimberly Guilfoyle, mwanahabari wa zamzni wa televisheni ya Fox News ambaye ni mpeziwe Donald Trump Jr, alikuwa ametembea Dakota Kusini kuiona familia ya Donald Trump Julai 4 na sherehe za fataki Mount Rushmore.

Guilfoyle, mwenye miaka 51 alitengwa baada ya kupimwa na kupatikana na virusi vya corona, iliripoti New York Times.

Katika habari aliyotoa Segio Gor mkuu wa wafanyakazi wa kamati ya kampeni na fedha ya Trump, “anaendelea vizuri na atapimwa tena ili kuhakikisha kwamba matokeo hayo yalikuwa ya kweli kwa sababu haonyeshi dalili zozote.”

Aliongezeza kwamba: “Ili kuzuia kusambaza virusi hivyo amefutilia mbali hafla zote..Donald Trump Jr hakupatikana na virusi hivyo lakini bado anajitenga.”

Bi Guilfoyle ni mtu wa tatu wa karibu na rais wa Marekani kupatikana na virusi vya corona.

Wengine ni mfanyikazi wa karibu wa Bw Trump na katibu wa wanahabari wa naibu wa Rais wa Marekani.

Watu 130,000 wamefariki Marekani kutokana na virusi vya corona .