Mwaniaji ubunge Embakasi Mashariki Francis Mureithi Wambungu aagizwa afike kortini kujibu shtaka la ulaghai wa Sh220Milioni za DOD

Mwaniaji ubunge Embakasi Mashariki Francis Mureithi Wambungu aagizwa afike kortini kujibu shtaka la ulaghai wa Sh220Milioni za DOD

Na RICHARD MUNGUTI

MWANIAJI kiti cha Ubunge cha Embakasi Mashariki kwa tikiti ya Chama cha Jubilee katika uchaguzi mkuu wa 2017 Francis Mureithi Wambugu ameagizwa afike kortini kujibu mashtaka ya ulaghai wa Sh220.8milioni kutoka idara  ya majeshi (DoD).N

Bw Wambugu aliagizwa afike mbele ya hakimu mwandamizi mahakama ya Milimani Bw Kennedy Cheruiyot mnamo Septemba 28,2021 kujibu mashtaka 11 ya ufisadi na ulaghai wa mali ya umma.

Bw Cheruiyot alitenga siku hiyo baada ya kusema kiongozi wa mashtaka hakuwa kortini.Bw Wambugu atashtakiwa pamoja Francis Mwaura Githenya.Wawili hawa wanakabiliwa na shtaka la kupokea pesa kwa njia ya undanganyifu.

Mabw Wambugu na Githenya wanashtakiwa kumfuja Haile Menkerios Dola za Kimarekani 2,208,000 (KSh220,850,000) wakidai kampuni yao ya Doc Find Company Limited ilikuwa imepewa zabuni na  Wizara ya Ulinzi kuuza bidhaa za vyakula kwa idara ya ulinzi (DoD).

Mabw Wambugu na Githenya wanadaiwa walipokea pesa hizo kati ya  Aprili 26 , 2016 na Novemba 1 2016.

Shtaka la pili ni dhidi ya Wambugu na lasema  mnamo Juni 20 2016 alinunua hisa katika kampuni ya CISCOS Kenya Limited na mashamba katika eneo la Ngong kaunti ya Kajiado za thamani ya Sh75milioni akijua pesa hizo zilikuwa zimepatikana kwa njia ya ufisadi.

Shtaka la tatu lasema mnamo Juni 21 2016 alinunua shamba katika eneo la Kaputiei kaunti ya Kajiado yenye thamani ya Sh51.5milioni.Shtaka hilo ladai mshtakiwa alijua pesa hizo zilikuwa zimepatikana kwa njia ya ufisadi.

Pia alikabiliwa na shtaka lingine la kununua jumba katika mtaa wa Kayole ya thamani ya Sh13.5milioni akitumia pesa alizopata kwa njia isiyo halali.Bw Cheruiyot alisema kwa vile kiongozi wa mashtaka hayumo itabidi washtakiwa arudi kortini Septemba 28 kujibu mashtaka.

Bw Wambugu aliwania kiti cha Ubunge cha Embakasi mashariki na kutwangwa na Bw Babu Owino.Bw Owino alipata kura 46,587 ilhali Bw Wambugu alizoa kura 42,253.Mahakama kuu iliratibisha ushindi wa Bw Owino.

  • Tags

You can share this post!

ULIMBWENDE: Njia rahisi za kutunza ngozi yako wikendi

AFYA: Umuhimu wa mtu kula chakula kwa uwiano unaotakiwa