Mwaniaji ugavana Kiambu aitaka serikali ihakikishe Wakenya wanamudu bei za vyakula

Mwaniaji ugavana Kiambu aitaka serikali ihakikishe Wakenya wanamudu bei za vyakula

NA LAWRENCE ONGARO

HALI ngumu ya maisha inastahili kutafutiwa suluhu kwa haraka na serikali licha ya viongozi kuendelea na kampeni zao.

Hali hiyo imesababisha hata wananchi kukosa kuhudhuria mikutano mingi ya kisiasa.

Mbunge wa Thika ambaye pia anawania kiti cha ugavana katika Kaunti ya Kiambu, Bw Patrick ‘Wajungle’ Wainaina, ameirai serikali kufanya jambo ili kuona ya kwamba wananchi wanapata chakula kwa bei nafuu.

“Katika misafara yangu niliyofanya Ngoliba, Ndula, Kilimambogo, na vitongoji vyake Thika Mashariki, nimepata ya kwamba wananchi wako katika hali ngumu ya maisha ambapo wanastahili misaada Ya chakula,” alifafanua Bw Wajungle.

Aliyasema hayo alipozuru vijiji tofauti akitafuta kuungwa mkono katika azma yake ya kuwania kiti cha ugavana wa Kiambu.

Bw ‘Wajungle’ anawania kiti hicho cha ugavana akiwa ameandamana na Bi Anne Nyokabi Gathecha, kama mwenza wake.

Mbunge huyo alitaka serikali iwe makini na kuona ya kwamba janga la njaa miongoni mwa Wakenya linatatuliwa haraka iwezekanavyo.

“Ninapozunguka katika kaunti yote ya Kiambu nimegundua ya kwamba wananchi wanapitia hali ngumu ya maisha hasa wale wanaolisha familia zao kila mara,” alieleza mbunge huyo.

Akaongeza: “Hata ingawa tunaelewa vyema ya kwamba matatizo kutoka mataifa ya kigeni yanasababisha masaibu yetu lakini pia serikali inastahili kujipanga kuona ya kwamba mwananchi angalau anapata kitu kidogo aweze kujikimu kimaisha.

Bw ‘Wajungle’ alipendekeza serikali itafute fedha za dharura kutoka Hazina Kuu.

Bw Wajungle ni mgombea wa kujitegemea baada ya kuangushwa kwenye uchaguzi wa UDA.

Kiti cha ugavana kimevutia wawaniaji watano Kiambu wakiwa ni Dkt James Nyoro (Jubilee), William Kabogo ( Tujibebe Wakenya Party), Kimani Wamatangi (UDA), na Moses Kuria (Chama cha Kazi) bila kumsahau ‘Wajungle’.

  • Tags

You can share this post!

Polisi wakamata washukiwa 81 na kutwaa silaha hatari Mtwapa

Ruto asema hana shida na maafisa wa IEBC

T L