Habari Mseto

Mwekezaji pabaya kwa kujenga jumba la Waititu bila idhini

August 15th, 2018 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MWEKEZAJI aliyefumaniwa akijenga jumba linalohusishwa na Gavana wa Kiambu Bw Ferdinand Waititu alishtakiwa Jumatano.

Bw Robert Rukwaro alikabiliwa na shtaka la kujenga jumba bila kuidhinishwa na idara ya ujenzi ya baraza la kaunti ya Nairobi.

Bw Rukwaro alishtakiwa muda mfupi baada ya mkewe Bw Waititu , kukanusha mashtaka ya kumiliki jumba bila leseni katika kwa kaunti ya Nairobi.

Bw Rukwaro aliyekanusha shtaka la kuendelea na ujenzi bila kibali kutoka kwa idara ya mipango na ustawi wa kaunti aliomba aachiliwe kwa dhamana.

Wakili Manases Mwangi aliymwakilisha mshtakiwa aliomba pia korti iamuru upande wa mashtaka uwakabidhi nakala za kesi ndipo aandae utetezi.

Kesi itatajwa Septemba 6.