Habari Mseto

Mwelekeo ni kozi za kiufundi – Nyutu

January 8th, 2024 1 min read

NA MWANGI MUIRURI 

MWENYEKITI wa Kamati ya Elimu katika bunge la Seneti Bw Joe Nyutu anasema shida kubwa ya elimu nchini ni ukosefu wa ajira.

“Nawashawishi wale watakaokosa nafasi katika vyuo vikuu wafikirie sana kujiunga na taaluma za kiufundi,” akasema.

Amesema hayo wakati wa utoaji rasmi wa matokeo ya KCSE 2023, Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu ambapo Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu anatarajiwa kuyatangaza.

Bw Nyutu amesema kwamba nafasi za kazi kwa uchumi wa sasa umeegemea kozi za kiufundi na kwamba serikali imezipa taasisi za kiufundi kipau mbele.

“Msiwe wa kurandaranda mitaani mkisema hakuna mianya ya kazi. Jiungeni na taasisi za kiufundi kwa kuwa serikali inatoa ufadhili wa Sh30, 000 kwa kila mwanafunzi,” akasema.