Mwendwa atupwa seli tena baada ya kukana mashtaka

Mwendwa atupwa seli tena baada ya kukana mashtaka

Na RICHARD MUNGUTI

RAIS wa Shirikisho la Kandanda Nchini (FKF) Nick Mwendwa, jana alipinga akishtakiwa kwa ubadhirifu wa zaidi ya Sh38milioni.

Kufuatia kupinga huko, hakimu mwandamizi Bi Eunice Nyutu aliamuru Mwendwa arudishwe tena rumande hadi leo atakapoamua ikiwa mashtaka manne ya ubadhirifu wa pesa za umma yatakubaliwa au la.

Mwendwa aliyekamatwa Ijumaa wiki iliyopita atazuiliwa tena kwa siku ya nne mfululizo katika kituo cha polisi cha Gigiri. Ombi la kupinga mashtaka hayo iliwasilishwa na mawakili Eric Mutua, Mutula Kilionzo Junior na aliyeeleza mahakama haki za Mwendwa zilikandamizwa na maafisa wa DCI waliomnasa.

ta kinara huyo wa kambumbu kiholela.“Mwendwa alianza kuhangaishwa Novemba 12,2021 kwa kukamatwa na kusukumwa rumande pasi kuzingatia haki zake kwa mujibu wa vifungu 47 na 50 vya Katiba vinavyojadilia kwa kina uzingatiaji wa haki,” alisema Mutua.

Mahakama ilielezwa Mwendwa alikamatwa baada ya waziri wa michezo Amina Mohamed kuteua kamati ya kuchunguza matumizi ya pesa za FKF.“Mwendwa amekamatwa kufuatia ripoti ya matumizi ya fedha za FKF ambayo iliandaliwa na kamati ambayo haikuwahoji maafisa wa FKF,” alisema Mutua.

Mahakama ilielezwa polisi wanamsumbua Mwendwa kwa vile FKF ilishtaki Serikali kufuatia kuteuliwa kwa kamati ya kusimamia shughuli za kandanda nchini kinyume cha sheria za mashirika ya CAF na FIFA.Mahakama ilielezwa Mwendwa alifikishwa kortini iliyopita na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh4milioni.

Mahakama ilitamatisha kesi dhidi ya Mwendwa Novemba 25 na keshoye akakamatwa.

You can share this post!

Washirika wa Ruto wadai Obado avuruga chama cha Naibu Rais

Wiki ya ubunifu yaanza rasmi

T L