Mwendwa kushtakiwa jumaa tatu

Mwendwa kushtakiwa jumaa tatu

Na RICHARD MUNGUTI

RAIS wa Shirikisho la Kandanda Nchini (FKF) Nick Mwendwa aliyekamatwa Ijumaa atashtakiwa Jumatatu kwa ubadhirifu wa pesa za umma.

Bw Mwendwa anayezuiliwa katika kituo cha polisi cha Gigiri atafikishwa katika mahakama ya Milimani kesho kujibu mashtaka. Alipokamatwa Ijumaa mwendo wa saa sita unusu kwenye barabara ya Kiambu akielekea jijini kutoka makazi yake mtaani Runda alipelekwa makao makuu ya uchunguzi wa jinai (DCI) kabla ya kuhamishwa hadi Gigiri anakozuiliwa.

“Polisi wametuhakikishia kwamba watamshtaki Jumatatu,” wakili Charles Njenga aliambia Taifa Jumapili kutoka kituo cha polisi cha Gigiri. Hata hivyo Bw Njenga hakufafanua kuhusu mashtaka zaidi akisema polisi watapeleka mashtaka afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma kuidhinishwa kisha yapelekwe kortini kusajiliwa.

Mnamo Novemba 25 2021 hakimu mwandamizi Bi Wandia Nyamu alimwachilia huru Mwendwa DPP alipokosa kuwasilisha mashtaka dhidi yake. Kiongozi wa mashtaka Bi Everlyne Onunga alisema jana afisi ya DPP inasubiri polisi wakamilishe uchunguzi kisha wamfungulie mashtaka Mwendwa.

“Tunasubiri polisi wakamilishe uchunguzi kisha wamfungulie shtaka Mwendwa,” Onunga alisema. Alipofikishwa mahakama wiki iliyopita DPP aliomba siku 14 polisi wakamilishe lakini uchunguzi lakini mawakili Eric Mutua, Prof Tom Ojienda, Dkt John Khaminwa na Silvia Matasi walipinga wakisema polisi wako na ripoti ya matumizi ya fedha za FKF,hawahitaji muda zaidi.

You can share this post!

Mahakama yakataa kuzima utoaji wa chanjo ya Covid-19 ya...

Shujaa yajizolea alama 10 Dubai 7s ikimaliza ya nane

T L