Habari Mseto

Mwezi mmoja kuwasilisha malalamishi yako kwa Kenya Power

October 23rd, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Wateja wa umeme wana mwezi mmoja kuwasilisha malalamishi kwa kampuni ya umeme ya Kenya Power.

Malalamishi hayo ni kuhusu makosa ya bili ya stima tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Wateja walio na malalamishi hawatatozwa ada ya kurejesha umeme katika kipindi hicho kama sehemu ya suluhu nje ya mahakama lililoafikiwa kati ya Kenya Power na wakili Apollo Mboya.

Bw Mboya alikuwa amewasilisha malalamishi mahakamani kwa niaba ya wateja wa umeme kuhusiana na bili kubwa ajabu walizokuwa wamepewa na Kenya Power tangu mwishoni mwa mwaka jana.

Kutokana na mkataba huo, Kenya Power ililazimishwa kutozwa wateja wake bili kuambatana na mapendekezo ya Tume ya Kawi nchini (ERC).

Kampuni hiyo pia itamlipa Bw Mboya na chama cha watumiaji wa umeme gharama ya kesi hiyo.