Kimataifa

Mwigizaji asimulia jinsi amekuwa akikwepa kifo

January 29th, 2019 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU

MWIGIZAJI mmoja kutoka Marekani ambaye ana miaka 76, amesema kuwa ‘amehadaa’ kifo mara tatu na kupona wakati alikaribia kufa zaidi, mwezi mmoja tu baada ya kuzirai, nusura afe.

Ken Morley aliugua alipokuwa akiigiza eneo la Panto, lakini anasema kuwa mbeleni amewahi kuugua saratani ya sehemu ya uume na magonjwa ya appendix. Hii, alisema ni licha ya kuugua moyo miaka kadha iliyopita.

Lakini alisema kuwa mafua ambayo yalimvamia majuzi yalikuwa na uchungu mwingi, hadi akadhani kuwa mwisho wake umewadia. “Ulihisi kama msumari wa mwisho kwenye jeneza,” akasema.

Hata hivyo, baada ya kupenya jaribio hilo, alisema anajihisi kama paka wanaodaiwa kuwa na roho tisa.

“Sijawahi kujihisi kukaribia kaburi kiwango nilihisi nilipokuwa nikitolewa jukwaani nilipokuwa panto, New York,” akasema.

“Nilipelekwa kwa ambulensi hadi hospitali, ambapo nililazwa siku tatu.”

Kwa sasa, Ken anazidi kupata nafuu nyumbani kwake Lancashire, huku akijiandaa kuandika kitabu kuhusu maisha yake ya sanaa kwa miaka 24.

Ken aliigiza mchezo wa ‘Celebrity Brother’ mnamo 2015, ambapo alipata kujulikana sana, na maneno yake yaliyoashiria uchafu kwa wanawake yakaibua kashfa na kupunguza mapato kwa takriban Sh10milioni.