Mwigizaji Michelle Wanjiku apania kufuata nyayo zake Lupita Nyong’o

Mwigizaji Michelle Wanjiku apania kufuata nyayo zake Lupita Nyong’o

NA JOHN KIMWERE

PENYE nia pana njia. Ndivyo wahenga walivyologa, na tangu zama zile baada ya kupasua hilo mpaka sasa, msemo huo ungali na mashiko katika jamii.

Pia ni msemo unaendelea kuthibitishwa na vijana wengi wavulana kwa wasichana wanaojitosa kuchangamkia shughuli tofauti kwenye jitihada za kusaka riziki. Michelle Wanjiku maarufu kama Mich ni miongoni mwa wana maigizo wa kike wanaoibukia wanaopania kutinga hadhi ya kimataifa miaka ijayo.

Mrembo huyu mwenye tabasamu ya kuvutia anasema ndio ameanza kupiga ngoma lakini amepania makubwa katika maigizo. Mich’ alianza kujituma kwenye masuala ya uigizaji kimzaha mwaka 2021.

Lakini mwaka jana 2021 alivutiwa zaidi alipotazama filamu iitwayo ‘Monica’ aliyongiza msanii Brenda Wairimu anayefahamika kwa jina Monica anapoigiza.

Kando na kipindi cha Monica ambacho kilipeperushwa kupitia Switch TV na Show Max, mwigizaji huyo anajivunia kushiriki vipindi kadhaa ikiwamo ‘Mali’ na ‘Selina’.

”Kwanza binafsi sikuwahi kuwazia kama ningeigiza maishani mwangu. Lakini kwa sasa ninajiona nikiwa ndani ya mwigizaji huyo ambapo nawazia makubwa ndani ya miaka ijayo,” anasema na kuongeza kuwa la mno aligundua kuwa uigizaji hulipa.

Anasema serikali inafaa kutufirikia zaidi na kutenga hela ndefu za kupaisha sekta ya uigizaji maana huwa tunatangaza nchi yetu kimataifa.

“Ingawa sijapata mashiko katika tasnia ya uigizaji, tayari ninafahamu wazi kuwa imeajiri wengi wanaume kwa wanawake,” anasema na kuongeza kuwa walioanza mapema wanastahili kukoma tabia uchwara ya kutaka kuzima ndoto za waigizaji wanaokuja.

Kwa waigizaji wa humu nchini anasema angependa kujikuta jukwaa moja na Sarah Hassan ambaye ameshiriki filamu zilizovuma kama ‘Crime and Justice’ pia ‘Zora’ ambayo hupeperushwa kupitia Citizen TV. K

isura huyu anayesema hana mpenzi hadi wakati mwafaka utakopowadia, anashikilia kuwa ndani ya miaka mitano ijayo amepania kutimiza ndoto ya kushiriki filamu nyingi za nguvu na kupata mpenyo kupeperushwa kwenye runinga.

Msanii chipukizi, Michelle Wanjiku. PICHA | JOHN KIMWERE

Ningependa sana kufikia hadhi ya mwigizaji wa kimataifa anayezidi kutamba kwenye filamu za Hollywood, Mkenya aliyezaliwa nchini Mexico, Lupita Nyong’o.

Kisura huyu anadokeza kuwa anapenda sana filamu yake iitwayo ’12 Years a Slave’.

Lupita amewatia motisha Wakenya wengi hasa waigizaji wa kike wanaokuja ambao kamwe hawajapiga hatua yoyote katika tasnia hiyo.

Lupita ameibuka kielelezo kizuri kwa waigizaji wengi tu wanaokuja. Amebahatika kuteuliwa kwenye tuzo kibao tangia atwae tuzo ya Oscar Awards mwaka 2012 kupitia filamu ya ’12 Years a Slave’.

Lupita amefanikiwa kuteuliwa kuwania tuzo nyingi tu ikiwamo: Golden Globe Award for Best Supporting Actress, a BAFTA Award for nest Actress, Screen Actors Guild Awards kati ya nyinginezo.

Mich’ amebahatika kushiriki kipindi cha ‘Closure’ ambacho hupeperushwa kupitia Ebru TV, ‘Date My family’ kupitia Maisha Magic pia ‘Pepeta’ katika Show Max TV.

  • Tags

You can share this post!

Mivutano yatishia kampeni za Ruto

CHARLES WASONGA: IEBC itoe maelezo muhimu kuhusu kura mara...

T L