Habari Mseto

Mwili wa aliyekufa maji akipiga picha wasakwa

August 2nd, 2020 1 min read

By STEVE NJUGUNA

Shughuli ya kumtafuta mwanamke ambaye alikufa maji alipokuwa akipiga picha akiwa na nduguye kwenye Thomson Falls mji wa Nyahururu kaunti ya Laikipia imeanza.

Jemima Oresha alikuwa amesimama juu ya jiwe karibu na mto Ewaso Narok alipotereza akanguka nani ya mto.Nduguye Zablon Mungafu alikuwa akimpiga picha wakati huo.

Bw Mungafu alisema kwamba Bi Oresha alisafiri kutoka Kitale kaunti ya Trans Nzoia Jumamosi kutembelea jamaa zake Nyahururu na alikuwa anatarajiwa kurudi Jumatatu.

“Jumapili alisema angerudi Kitale kabla ya kutembelea kivuto maarufu cha watalii ,”alisema Bw Mungafu.

“Tulipofika hapo alifurahia sana na kuniomba nimpige picha akiwa amesimama njuu ya jiwe karibu na mto,mita mbili kutoka nilipokua. Nilikuwa nimemaliza kupiga picha alipokuwa akirudi nilipokua alitereza na akaanguka ndani ya mto na akabebwa na maji nikiangali.Singefanya lolote kwanimaji ilikuwa inaenda kwa kasi.”