Habari

Mwili wa bwanyenye Tob Cohen wapatikana katika tanki kwake Kitisuru

September 13th, 2019 1 min read

Na JOHN KAMAU

HATIMAYE maafisa wa polisi wamefanikiwa kuupata mwili wa bwanyenye Tob Cohen katika tanki la majitaka nyumbani kwake Kitisuru, Nairobi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Makosa ya Jinai (DCI) George Kinoti, mwili wa Mholanzi huyo umepatikana Ijumaa mchana ukiwa umetupwa kwa tanki hilo nyumbani kwake.

Akiwa na umri wa miaka 71, Cohen ambaye alikuwa mtaalamu wa huduma za ziara na usafiri alikuwa na matatizo ya kifamilia ambapo kulikuwa na kesi ya talaka dhidi ya mkewe ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi Sarah Wairimu Kamotho.

Marehemu pia alikuwa amewasilisha kesi mahakamani dhidi ya mke wake kuhusu udhalilishaji.

Kutoweka kwa Cohen

Bw Cohen alitoweka baina ya Julai 19 na 20 na Kamotho alikuwa ameambia wachunguzi kwamba mumewe alikuwa amesafiri kuenda Thailand.

“Alisema anaenda mapumzikoni,” mkewe Cohen aliambia Taifa Leo awali.

“Mawakili wanamsukuma wakitaka pesa na alitaka kuenda kupata matibabu.”

 

Tunaandaa habari kamili…