Habari Mseto

Mwili wa kijana aliyekufa maji wapatikana

November 14th, 2020 1 min read

NA CHARLES WANYORO na FAUSTINE NGILA

Mwili wa kijana wa miaka 13 aliyekufa maji kwenye bwawa la Kianjuti kwenye eneo la Marania Buuri Magharibi Kaunti ya Meru siku tisa zizlizopita umepatikana baada ya kutafutwa kwa muda.

James Mwenda,mwanafunzi wa  darasa la saba kwenye shule ya msingi ya Ntiriminti alikuwa akikimbiza  dama alipokuwa akilisha ndipo aliingia kwenye bwawa hilo lenye urefu wa mita 300,000.

Vijana wezake waljaribu mvuruta kumwokoa bila mafanikio.

Wapiga mbizi walitafuta mwili huo bila mafanikio huku ikiwalazimu Kserikali ya Kaunti ya Meru kuingililia kati kwa kutumia wapiga bizi kutoka Kaunti ya Mombasa.Wazazi wa kijana huyo walijawa na huzuni kwani ata hawakuungalaia mwili wa mwanawao.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Ntirimiti  Moses Koome alimwomboleza kijana na kumtaja kuwa alikuwa kijana aliyekuwa na talanta.