Habari Mseto

Mwili wa mkurugenzi hatimaye wapatikana

October 7th, 2020 1 min read

NA STEPHEN MUNYIRI

Mwili wa aliyekuwa mkurugenzi wa kiwanda cha majani chai cha Ragati, Wilfred Murigu ulipatikana Jumanne kwenye mto wa Sagana siku sita baada ya kupotea.

Gari lake lilipatikana kando ya barabara ya Karatina kuelekea Mukurweni karibu na daraja la Gatiki.

Koti alilokuwa amevalia siku alitoweka pamoja stakabathi zake zilipatikana zikiwa sawa. Polisi walisema simu yake haikupatikana.

Mpelelezi wa DCI Mathira Mashariki  alisema kwamba uchunguzi unaendelea kubaini nini kilichoelekea kifo cha Bw Murigu.Bw Murigu alipoteza nafsi yae ya ukurugenzi kwenye kiwanda hicho cha majani chai miezi mbili iliyopita.

Bw Mutinda alisema kwamba vyenye ishara za simu yake ilipofuatiliwa zilionekana Mwea kaunti ya Kirinyanga kilonita 100 mbali hili likiashiria kwamba Bw Murigu kuna uwezekno aliuliwa.

“Kifo chake bado hakijajulikana kilisababishwa na nini.Tunachunguza kila pande kubaini kilichosababisha kifo hicho.Tulidhania alijitia kitanzi lakini kuna uwezekano si hio,”aliambia Taifa Leo.

“Hatuwezi tukabaini kilichoeleke kifo chake kwani stakabathi zake Kadi za ATM na akaunti za benki ziko sawa hazijaharibiwa.

Mwili wake ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha Karatina Jamii.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA