Habari Mseto

Mwili wa msichana aliyekufa maji Rangwe bado wasakwa

November 16th, 2020 1 min read

GEORGE ODIWUOR NA FAUSTINE NGILA

Familia   moja eneo la Kochia ya Kati Kaunti ndogo ya Rangwe imekuwa ikitafuta mwili wa msichana wao wa miaka 10 aliyekufa maji  siku tatu zilizopita kwenye mto Awach Ijumaa.

Shughuli ya kuutafuta mwili wa msichana huyo ambaye alikuwa mwanafunzi wa shule ya msingi ya Nyarut inaendelea.

Msichana huyo aliyetambulika kwa majina Quinter Achieng alitereza na kuanguka ndani ya mto alipokuwa akicheza na marafiki zake karibu na kando yam to huyo.

Bw Frederick Otieno baba ya msichana alisema kwamba mwili ya msichana  labda huyo labda ulibebwa hadi ziwa Viktoria na mawimbi.

Wapiga mbizi kutoka kijijini wamekuwa wakitafuta mwili huo lakini wamepata matatizo ya maji yaliojaa matope.

Kukosekana kwa wapiga mbizi wenye ujuzi kuathiri shungli hiyo ya kutafuta mwili.

Familia hiyo inahofia kwamba watakosa kukosa mwili huo kama hawatapata usaindizi kutoka kwa serikal  ya Kaunti.