Habari Mseto

Mwili wa msichana ambaye mamake alijirusha mtoni wapatikana

May 5th, 2024 1 min read

Na GEORGE MUNENE

MWILI wa msichana mwenye umri wa miaka mitano ambaye alizama kwenye mto Nyamidi, Kaunti ya Kirinyaga na mamake umepatikana Jumapili.

Kisa hicho kilichosababisha mauti ya dogo huyo na kilichoshangaza kilitokea mnamo Jumamosi na mwili wa mamake nao bado haujapatikana.

Kamanda wa Polisi John Wachira alisema mwili wa mtoto huyo ulipelekwa katika hifadhi ya maiti huku mwili wa mamake nao ukiendelea kutafutwa.

Mwanamke huyo alijificha na akiwa amemfunga mwanawe mgongoni alijitumbukiza kwenye mto Nyamidi ambao umefurika na kuvunja kingo zake.