Habari Mseto

Mwili wa msichana wapatikana bila macho na ulimi

February 6th, 2020 2 min read

NA MERCY KOSKEY

[email protected]

WAKAZI wa mtaa wa Kaptebwa, Kaunti ya Nakuru waliamkia kisa cha kushangaza hapo baada ya mwili ya msichana mdogo kupatikana akiwa ameuwawa na kutupwa kwenye timbo.

Mwili huo wa mtoto mwenye umri ya kati ya miaka 13 na 15 haukuwa na macho, ulimi na pia uso wake ulikua umechomwa kiasi cha kukosa kutambuliwa.

Inasemekana kuwa vijana ambao wanafanya kazi ya kuchimba mchanga kwenye shimo hilo ndio walikua wa kwanza kuupata kabla ya kupiga ripoti kwa mzee wa mtaa wa eneo hilo.

Maafisa wa polisi walikua na wakati mgumu kudhibiti mamia ya watu waliofika kutoka vijiji vya Rhonda, kaptebwa, Nakuru west na soko mjinga kushuhudia kisa hicho.

Mamia ya wakazi walijitokeza kushuhudia polisi wakitwaa mwili huo. Picha/ John NJoroge

Bi Jane Kemunto, mkaazi wa eneo hilo alisema kuwa alipigwa na butwa alipoona watu wengi wakielekea kwenye mahala pa kisa na ivo kumfanya kuuliza kile ambacho kimetokea.

“Nilikua nafanya kazi zangu za nyumba ikanilazimu kuacha. Nilipofika hapa nilishtuka kupata mwili wa mtoto umetupwa hapa baada ya kuuwawa,” alisema Bi Kemunto.

Hata hivo aliomba uchunguzi iweze kufanywa haraka ili wale waliotekeleza uhovu huo waweze kukamatwa ndiposa sheria iweze kufuata mkondo wake.

“Tuna wasiwasi mwingi sana kwa yale ambayo yametokea leo. Tungeomba serikali iweze kuimarisha usalama eneo hili visa kama hizi ya mauaji viweze kuzuiwa,” aliongeza.

Mwenyekiti wa sera ya jamii ya Kaptembwa Bw James Koskei alisema kuwa alipata habari hiyo kutoka kwa mmoja wa wachimba mchanga akimweleza yale ambayo yametokea.

Alisema kuwa aliweza kupiga ripoti kwa afisa wa usalama ili waje wachukue mwili.

“Visa kama hivi vilikua vimepungua. Tungeomba polisi iweze kuimarisha usalama upande huu.Tunahofia Maisha yetu sasa,” alisema Koskei

Kulingana na Bw Koskei wanashuku kuwa msichana huyo uliuliwa mahala pengine na mwili wake kutupwa mahala hapo.

“Ni vingumu kumtambua kwani uso wake umechomeka. Tunaomba yeyote ambaye amepoteza mpendwa wao aweze kupiga ripoti kweye kituo cha polisi,” alisema Koske.

Hata hivo aliomba wakaazi wa Nakuru waweze kuwa wangalifu akati wowote na kupiga ripoti wakishuhudiwa hali isiyo ya kawaida.