Habari Mseto

Mwili wa msimamizi wa majanichai wapatikana kando ya barabara

May 25th, 2020 1 min read

NA MWANDISHI WETU

Wakazi wa Kirinyaga wameachwa na mshuto baadaya ya mfanyikazi wa kiwanda cha majani chai kupatikana ameuwawa na mwili wake kutupwa kando ya barabara Jumapili asubuhi.

Polisi walisema kuwa mwili wa Albert Mwangi mwenye miaka 51 ulikuwa na maumivu kichwani. Alikuwa akifanya kazi kama msimamizi katika kiwanda cha majani chai cha Thumaita.

“Inakisikiwa kwamba Mwangi aliuwawa kwingine na mwili wake kutupwa mita 200 karibu na kiwanda hicho ili kuficha ukweli,” wakasema.

Alitoka kwa kiwanda Jumamosi na akapatikata amekufa Jumapili asubuhi saa moja.

Akithibitisha kisa hicho, mkuu wa polisi Antony Wanjuu eneo la Kirinyaga Kaskazini alisema kuwa alipata habari hizo kupitia kwa naibu chifu wa eneo hilo.

“Tulipashwa habari hizo na naibu wa chifu kua mfanyakazi huyo alikua ameuwawa na watu wasiojulikana. Hapo ndipo tulimkimbiza kwenye chumba cha kuhifadhi maiti kwa uchunguzi zaidi,”alisema.

Bw Wanjuu alisema uchunguzi unaendelea ili kubaini kiini cha mauaji hayo. Aliwaomba wananchi wakipata habari zozote wawajulishe polisi ili wanaohusika watiwe mbaroni.

Wakazi walisema kuwa kifo hicho ni cha kusitikisha na wangeomba polisi wafanye uchunguzi kamili.

“Tungependa kujua aliyemuua Mwangi na nia yake ya kumuua,” mmoja wa wakazi alisema.

Tafsiri: Faustine Ngila