Habari Mseto

Mwili wa mvulana aliyeuawa na mamba wapatikana

June 2nd, 2020 1 min read

By ALEX NJERU

Familia moja katika Kijiji cha Maraja kaunti ndogo ya Tharaka inaomboleza baada ya mwanao wa kiume alipouwa na mamba katika Mto  Tana.

Mwili wa mvuana huyo, Munyambu Mutira ulipatikana baadaye baada ya kufa maji alipokabiliwa na mamba.

Katika tukio hilo kijana huyo alikua na mwenzake aliyejaribu kumuokoa lakini ikashindikana. Chifu wa eneo la Maragwa William Kwenga alisema si mara ya kwanza wakazi kuvamiwa na mamba.

Alisema kwamba maafisa wa Wanyama wa porini kutoka bunga la Meru walitembelea eneo hilo huku wakionya wanachi kutowaruhusu watoto kutembea kwa mito yenye mamba na viboko..

Aliwashauri familia ya kijana huyo kukiripoti kisa hicho kwa polisi na kujaza fomu ya fidia.

Mkazi wa eneo hilo Njagi alisema kwamba watoto watano wamepoteza maisha yao ma mamia ya mifugo kuuawa na mamba miaka iliyopita. Aliirai serikali kutoa maji kwa wananchi na maeneo ya kunywesha mifugo.