Habari Mseto

Mwili wa mwanafunzi aliyetoweka wapatikana kando ya mto

October 25th, 2020 1 min read

George Munene na Faustine Ngila

Mwili wa mwanafunzi wa shule ya upili aliyepotea kwa muda wa siku tatu ulipatikana umetupwa kando ya mto katika kijiji cha Kanagru, Kaunti ya Embu.

Mwnafunzi huyo wa kidato cha pili aliyetambulika kama Immanuel Derick wa miaka 17 alikuwa na majeraha ya kudungwa shigoni kumaanisha kwamba alivamiwa kabla ya kifo chake.

Kufuatia maujai ya kijana huyo maafisa wa DCI wanafanyauchunguzi kutafuta kilichoelekea mauaji yya kijna huyo na ni kwanini aliuliwa.

Mwanafunzi huyo alipotea nyumbani kwao Kijiji cha Gakwegori Oktob 18,2020 na alipatikana amefariki Jumatano.

Mwili wa kijana huyo ulipatikana na wanakijiji ambao waliripoti kisa hicho kwa kituo cha polisi cha Itabua..

Hapo ndipo polisi walienda eneo hilo na kuchukua mwili na kuupeleka kwenye chumba cha maiti Enbu kwa upasuaji.

Kulingana na wazazi wa kijana huyo walienda kanisa wakamuacha nyumbani na waliporudi jioni hawakumpata.

Mamayake Roselyne Muthoni alisema kwamba kifo cha mwanawe kilimshtua sana.

“Alikuwa mwana wa pekee na wakati nilipata Habari kuhusiana na kifo chake nilikuwa karibu nizirahi,”aliambia Taifa Leo.

Wazazi wake walipogundua kupotea kwa kijana huyo walimatafuta kila mahali bila kumpata.

Wazazi wake walisema kwamba walishuku kwamba kitendo kibaya kilikuwa kimetendekea mwanawao wakati simu yake ilikosa kushikwa.