Habari Mseto

Mwili wa mwanamke aliyekufa maji waendelea kusakwa

September 2nd, 2020 1 min read

Na Titus Ominde

Mwili wa mwanamke aliyekufa maji walipokuwa wametalii kivutio cha maji cha Chepkitii akiwa na mpenziwe kwenye mpaka wa kaunti ya Uasin Gishu na Nandi bado hujapatikana.

Familia yake Dorcus Jepkemboi Chumba mwenye umri wa miaka 31 kutoka Jumapili imekuwa ikitafuta mwili huo bila mafanikio.

Bi Chumba anaishi Kipsao Keiyo Kusini. Alibebwa na maji alipokuwa ametembelea eneo hilo la kivutio akiwa na mpenziwe.

Juhudi za kutafuta mwili huo na wapiga mbizi waliojitotela kuutafuta hazijazaa matunda kwasababu ya mvua kubwa inayoshuhudiwa sehemu hizo.

Timu ya Kaunti na polisi iliwachia shughuli hiyo familia na wapiga mbizi wa kujitolea.

Bw Kiptoo Chelego,babake Bi Chumba alieleza kutoridhishwa na jinsi polisi na serikali ya kaunti ilichukulia msimba huo uliowakumba.

Baba huyo wa Watoto tisa alisema kwamba licha ya kisa hicho kuripotiwa kwenye kituo cha polisi cha Mosoriot maafisa hao wa polisi walitembelea eneo la tukio Jumatatu pekee siku tatu baada ya tukio.

“Nilikuja kwenye eneo la tukio Jumatatu asubuhi kulikuwa na wakazi pekee na watu wa familia nilipouliza polisi walisema walikuwa wanaomboleza kivyao wakiwa kwenye kituo cha polisii huku sisi tukiwa tutaombolezea kwenye eneo la tukio,”alisema Bw Chelego.

 

Tafsiri na Faustine Ngila