Dondoo

Mwoshaji choo akemea kipusa kwa kukataa kumsalimia kwa mikono

February 20th, 2024 1 min read

NA NICHOLAS CHERUIYOT

TENWEK, BOMET

JOMBI anayefanya kazi kama chura katika shule moja ya eneo hili alimfokea kipusa mmoja kwa kudinda kumpa mkono kumsalimia.

Inaarifiwa kuwa polo alikuwa ameng’ara baada ya kumaliza kazi zake asubuhi alipokutana na kidosho huyo.

“Jamaa alinyoosha mkono kumsalamia kipusa huku tabasamu likiwa usoni mwake. Kidosho akakunja mikono yake na kumjibu polo tu kwa mdomo kisha akapita kwa haraka,” mdaku akaarifu.

“Unafikiria mimi ni mchafu? Huoni nimeoga baada ya kufanya ile kazi yangu ya kawaida. Acha maringo,” polo alifoka kwa hamaki.

Kipusa aliongeza mbio kuhepa jamaa huyo naye akazidi kulia kuwa alidharauliwa kwa kuwa yeye ni hasla anayeng’arisha vyoo.