Habari Mseto

Mzee adaiwa kumuua mwanawe katika mzozo wa shamba Kirinyaga

February 6th, 2024 1 min read

NA MWANGI MUIRURI

MZEE wa umri wa miaka 70 katika Kaunti ya Kirinyaga amekamatwa baada ya kuripotiwa kumuua mwanawe kwa kumdunga kisu baada ya mzozo kuzuka kuhusu urithi wa shamba.

Ripoti ya polisi inaelezea jinsi James Muobe Njagi,32, alivyodaiwa kudungwa kisu rohoni na babake Francis Njagi Kibaki katika kijiji cha Karumandi mnamo Jumapili.

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika mochari ya Kerugoya.

Polisi walisema mzee huyo atashtakiwa kwa mauaji.