Habari Mseto

Mzee akana ulaghai wa hatimiliki ya shamba Kawangware

May 22nd, 2018 1 min read

David Wanyee Kamuyu akiwa kiziambani kwa ulaghai Mei 21, 2018. Picha/ Richard Munguti

Na RICHARD MUNGUTI

BABU wa miaka 75 ameshtakiwa  kwa ulaghai wa shamba lenye thamani ya Sh500,000 mtaani Kawangware, kaunti ya Nairobi.

David Wanyee Kamuyu alikanusha shtaka la kumlaghai Pascal Odhiambo ardhi yake.

Alishtakiwa kwamba mnamo Mei 15, 2017 katika mtaa wa Kawangware eneo la uwakilishi bungeni la Dagoretti, kaunti ya Nairobi alighushi nambari ya umiliki wa ardhi ya Bw Odhiambo

Bw Kamuyu aliyeandamana kortini na wanawe watatu wote wakiwa wamefunga vilemba, aliomba hakimu amwachilie kwa dhamana.

“Mzee huyu hawezi kutoroka. Alikuwa ameachiliwa na polisi kwa dhamana ya Sh5,000 pesa tasilimu. Alijileta kortini, anaheshimu sheria. Naomba umwachilie kwa kiasi sawa na hicho alichokuwa amepewa na polisi,” wakili  Boniface Njiru anayemwakilisha alieleza mahakama.

Bw Cheruiyot aliamuru mshtakiwa aachiliwe kwa dhamana ya Sh5,000 pesa taslimu.