Kimataifa

Mzee aliyejigamba kutafuna wanawake 6,000 afariki akimumunya uroda

February 5th, 2019 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU

MZEE tajika wa miaka 63 nchini Italia ambaye amefahamika sana kwa kujihusisha kimapenzi na wanawake wengi na ambaye anadaiwa amefanya ngono na zaidi ya wanawake 6,000 alifariki akifanya ngono na mwanamke wa miaka 23.

Bw Maurizio Zanfanti ambaye alifahamika zaidi kama Romeo wa Rimini anadaiwa kulala na idadi yote hiyo ya wanawake tangu miaka ya ’70 alipotambulika katika klabu moja jiji la pwani.

Lakini Jumanne wiki iliyopita alipokuwa akijiburudisha na mwanamke mtalii kutoka Romania alipatwa na mshtuko wa Moyo na akafariki.

Kwa mshangao mkubwa, mwanamke huyo anadaiwa kuwaita madaktari, lakini Zanfanti akawa tayari amekata roho.

Mashirika ya habari ya nchi hiyo, hata hivyo, yaliripoti kuwa mzee huyo aliyefahamika kama “mpenzi aliyefanikiwa sana Italy” alitaka kuaga dunia katika hali hiyo.

“Zanza alifariki baada ya kufanya kile alichopenda sana- kuwapa uroda wanawake,” gazeti moja la Italy likachapisha.

Meya wa mji wa Rimini naye alisema kuwa Italy imepoteza “shujaa wa usiku.”

Zafanti alianza kazi yake ya mapenzi na wanawake wengi alipokuwa na miaka 17, mnamo 1972 wakati alipokuwa akifanya kazi katika klabu ya usiku.

Kazi yake katika klabu hiyo ilihusisha kuwavuta watalii kutoka Ujerumani na Scandinavia kuingia katika klabu yao, wakiwa barabarani.

Kutokana na maumbile yake ya utanashati, hakuwa na wakati mgumu kuwavuta.

Alijigamba kuwa misimu ya baridi aliweza kulala na hadi wanawake 200.

Mnamo 1986, gazeti moja la Italia lilimpa jina “mpenzi aliyefanikiwa sana Italia”

Mnamo 2014, hata hivyo, alitangaza kustaafu katika kazi hiyo na kusema kuwa “nikiwa miaka 59 najihisi nimezeeka sana kwa kazi hii.”

Lakini kama mustakabali ulivyopanga, Jumanne wiki iliyopita aliaga dunia, japo akifanya ngono na mwanamke aliyemzidi kwa miaka 40.