Mzee Oroni bado anatimua mbio hafikirii kustaafu licha ya umri wake wa miaka 69

Mzee Oroni bado anatimua mbio hafikirii kustaafu licha ya umri wake wa miaka 69

NA JOHN ASHIHUNDU

LICHA ya umri wake mkubwa wa miaka 69 na uhusiano duni dhidi ya Shirikisho la Riadha Kenya (AK), mzee Reuben Oroni anazidi kutoa upinzani mkali katika mbio za marathon za wazee, almaarufu Masters.

Mzee Oroni ni mtu wa kwanza kutoka katika jamii ya Teso kumaliza mbio hizo za kilomita 42 katika muda wa 2:19.32, alipokimbia mbio za Kilimanjaro International Marathon akiwa na umri wa miaka 65.Oroni aliibuka mshindi wa mbio hizo zilizojumuisha wakimbiaji wa kuanzia umri wa miaka 40 hadi 99, akifuatiwa na Mtumba Chumps wa Tanzania na Kariuki Karanja waliomaliza kwa muda wa 2:31.12 na 2:53.22 mtawaliwa.

Lakini licha ya uwezo wake kwa kuletea Kenya sifa za kimataifa, mwanariadha huyo amekuwa na uhusiano mbaya na AK, kiasi cha kunyimwa nafasi ya kuwakilisha Kenya katika mbio hizo kule ng’ambo.Oroni anakumbukwa kwa kuwa miongoni mwa wanariadha maarufu kama Ben Jipcho, Kipchoge Keino, Naftali Temu na Elkana Nyang’au ambao pia waliwahi kuiletea Kenya sifa kutoka na ushindi wao katika mbio mbali mbali za kimataifa.

Baada ya kunyimwa cheti cha kushiriki mbio tisa katika mataifa ya kigeni yakiwemo Uingereza na Uhispania, mzee Oroni aliyemaliza katika nafasi ya pili kwenye mbio za kitaifa zilizofanyika 2018 kule Kasarani anajihusisha na mbio za kuleta Amani kule Kitale chini ya udhamini wa Askofu Maurice Croly wa Dayosisi ya Kitale.

Anapanga kuandaa mbio za Peace Foundation for Hunger kutoka Mlima Tororo hadi Ikulu, Nairobi ambako anatarajia kupokelewa na Rais Uhuru Kenyatta.

You can share this post!

Samaki waoza kwa ukosefu wa jokofu la hifadhi

TAHARIRI: Aina mpya ya Covid ikabiliwe isilete lockdown

T L