Habari Mseto

Mzee wa miaka 60 ndani kwa kumdhulumu kimapenzi msichana wa miaka 13

October 18th, 2020 1 min read

NA WAWERU WAIRIMU

Korti imeruhusu polisi kumzuilia mzee wa miaka 60 aliyemuoa msichana mchanga eneo la Biliqo, kaunti ndogo ya Merti, Isiolo ili kufanya uchunguzi zaidi.

Bw Ali Matamolu alikamatwa siku chache baada ya Rachel Shebesh kuzuru eneo hilo. Alisema alichukizwa na maafisa wa usalama kuchelewesha mchakato wa kuchukua hatua dhidi yake.

Bi Shebesh alisema kwamba Bw Matamolu alikamatwa wiki mbili baada ya msichana huyo kuokolewa na kikundi cha Somalia  ambacho mwenyekiti  wake ni Fani Mohammed.

Mshukiwa huyo alifikishwa kortini Ijumaa na kushatakiwa kwa kumdhulumu kimapenzi msichana huyo kati ya Novemba 27 na Desemba 30 2019.

Ripoti zilisema kwamba Bw  Matamolu alianza kuishi na msichana huyo wa miak 13 ambaye ni wa darasa la tatu wakati shule zilifungwa Machi.

Alikana madai hayo alipofikishwa mbele ya hakimu mkuu wa Isiolo Evanson Ngigi.

Msichana huyo aliokolewa alipokuwa akitafuta kazi baada ya kutoroka kwa mwanamume huyo kilomita 230 kutoka mjini Isiolo.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA