Mzozo mpya watokota Mumias Sugar

Mzozo mpya watokota Mumias Sugar

Na BRIAN OJAMAA

MZOZO mpya umeibuka katika Kampuni ya Sukari ya Mumias, baada ya wakulima kushinikiza kubadilishwa kwa usimamizi wa kampuni hiyo.

Kwa miezi kadhaa iliyopita, kampuni hiyo imekuwa ikikumbwa na changamoto za kifedha.

Wakulima wanaulaumu wasimamizi kwa kutoanza shughuli zake rasmi, ili kuwalipa deni la zaidi ya Sh70 milioni linalotokana na miwa waliyopeleka.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa Chama cha Wakuzaji Miwa wa Nzoia (NOUC), Bw Christopher Sifuna, wakulima hao walivamia afisi za kampuni wikendi iliyopita, ambapo walijaribu kumwondoa afisini Mkurugenzi Mkuu, Bw Michael Makokha kwa nguvu.

Hata hivyo, ililazimu Mbunge wa Kanduyi, Wafula Wamunyinyi kuingilia kati, ambapo aliandaa kikao cha dharura kati ya wakulima na wasimamizi hao kuhusu namna ya kusuluhisha mzozo huo.

“Wiki mbili zilizopita, tuliipa kampuni siku 14 kuwalipa wakulima fedha zao na muda huo umeisha,” akasema Bw Sifuna.

You can share this post!

Jaji Nderi aelezea sababu ya kutoroka Kenya

Wamiliki hoteli wapinga ushuru wa vitanda