Nafula atinga bao AE Larissa ikishinda shaba kwenye Ligi Kuu ya Ugiriki

Nafula atinga bao AE Larissa ikishinda shaba kwenye Ligi Kuu ya Ugiriki

Na GEOFFREY ANENE

KIUNGO mshambuliaji wa Kenya, Christine Nafula alisaidia AE Larissa FC kutamatisha Ligi Kuu ya Ugiriki ya msimu 2020-2021 na medali ya shaba Jumapili.

Nafula alitikisa nyavu mara 12 ligini katika msimu wake wa kwanza baada ya kutikisa nyavu mara moja katika ushindi wa Larissa wa 2-0 dhidi ya Agia Paraskevi katika mechi ya kuamua nambari tatu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, ambaye alijiunga na Larissa katikati mwa msimu kutoka Dalhem IF nchini Uswidi mwezi Machi, aliona lango dakika ya 71. Ribanska alikuwa ameweka Larissa kifua mbele 1-0 dakika ya 31.

Mechi hiyo ilikutanisha timu mbili zilizomaliza makundi yao ya ligi katika nafasi ya pili. Larissa ilikamilisha Kundi A nyuma ya PAOK nayo Paraskevi ikawa ya pili Kundi B nyuma ya Chalkidas. PAOK ilizaba Chalkidas 2-0 kuhifadhi ubingwa. Mechi hizo zilisakatiwa ugani Panthessaliko.

You can share this post!

Uholanzi wakanyaga Ukraine 3-2 kwenye Euro

Zesco United yanyanyua taji la Ligi Kuu Zambia