Naibu chifu ajivunia usalama katika kaunti ndogo ya Chonyi baada ya sifa mbaya

Naibu chifu ajivunia usalama katika kaunti ndogo ya Chonyi baada ya sifa mbaya

NA MAUREEN ONGALA

NAIBU Chifu wa Mwembekati Bw Mwambolo Mwambao amejivunia usalama ambao ulishuhudia katika eneo hilo na kaunti ndogo ya Chonyi katika uchaguzi mkuu.

Kulingana na Bw Mwambao eneo la Chonyi limejulika kwa ukosefu wa usalama wakati wa uchaguzi mkuu kuanzia mwaka wa 2013, kufatia kuwepo kwa kundi la Mombasa Republican Council (MRC).

Kulinga na Bw Mwambolo,utulivu huo ulishuhudiwa kufatia juhudi kambambe za kuimarisha usalama kutoka kwa maafisa wa serikali ya utawala, viongozi wa dini, jamii pamoja na shirika lisilo la serikali la Kenya Community Support Centre (KECOSCE).

Viongozi hao waliandaa mikutano ya amani na usalama katika kata ndogo tisa za Chonyi wakilenga lenga vijana ambao walikuwa mstari wa mbele vuzua vurugu wakati wa uchaguzi mkuu.

Vijana hao walijiunga kwa magenge na makundi mengi ikiwemo kundi la Mombasa Republican Council (MRC)ambalo halikuunga mkono uchaguzi mkuu kwa madai ya kuwa eneo la Pwani lilikuwa limetengwa kimaendeleo na wenyeji walipitia dhuluma mingi ikiwemo ukosefu wa mashamba ambalo lilichangia wao kuwa maskwota.

Akizungumza na Taifa Leo ofisini mwake, Bw Mwambolo alisema kuwa ukosefu wa usalama katika eneo la Chonyi iliipea sifa mbaya huku jamii hiyo ikikosa kushuhudia maendeleo na uongozi bora kwa muda.

“Wakati wa miaka iliyopita eneo la Chonyi ilikuwa ikitajwa vibaya kila wakati wa uchaguzi mkuu sababu ya uhalifu ambao ulikuwa unatokea.Lakini mwaka huu tulishikana vizuri na wananchi lengo likiwa kuhakikisha kuna uchaguzi wa amani.

Tumeshuhudia kwa mara ya kwanza eneo la Chonyi ilikuwa na uchaguzi mkuu wa amani,” akasema.

Bw Mwambao alisema kuwa kundi la MRC lilitajwa kutekeleza vurugu, mauji na uharibu wa mali ya serikali ikiwemo kuchoma magari wakati wa uchaguzi mkuu wa 2013.

Naibu wa Chifu alieleza kuwa ilikuwa vigumu wakazi kusafiri na hata kwenda shambani kukuza chakula kwa ya kuhofia kuvamiwa na MRC.

“Kundi hilo lilileta madhara kubwa na Chonyi ikaa zaidi ya miaka mitatu bila kuwa na Afisa mkuu wa utawala na kazi ya utawala ilikuwa ngumu kupata afisa ambaye alikuwa radhi kufanya kazi huku na pia hakuna polisi alitaka kuja huku,” akasema.

Hata hivyo hatua ya serikali ya kitaifa kuifanya eneo la Chonyi kuwa kaunti ndogo ilisaidia kuregesha hadhi ya jamii ya wachonyi na jamii hiyo ilishuhudia maendelo pakubwa.

Bw Mwambao alisema kuwa hapo awali jamii walisafiri kwa mwendo mrefu kutafuta huduma za serikali kuu Kikambala, makao makuu ya eneo bunge la Kilifi Kusini.

Vijana walisafiri hadi Kikambala wakati wa zoezi la kuchagua makurutu katika jeshi, polisi na hata Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS).

“Tulikuwa tunateseka zamani kwa sababu vijana wengi walienda katika majaribio ya kutafuta kazi lakini hatukwa tunapata idadi ya kuridhisha kutoka lokesheni nne za Chonyi,” akasema.

Alieleza kuwa wakazi wa Chonyi wanatazamia kuona mabadiliko makubwa kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Afisi za kutoa hati za kuzaliwa, elimu na huduma za watoto ni miongini mwa zile zinatoa huduma za muhimu kwa jamii.

“Wanachi wanahudumiwa hapa na wanaridhika. Tunatamani mambo mengi mazuri yatafanyika tukizingatia kuwa tumeingia katika serikali mpya,” akasema.

Alitoa wito kwa jamii ya Chonyi kufanya kazi na serikali ya utawala na vyombo vya usalama kuendeleza amani kila wakati.

Pia kujituma kwa maswala ya maendeleo ikiwemo kukuza chakula ili kupigana na baa la njaa, kuepuka na maswala ya kuangamiza wazee kwa madai ya uchawi na migogoro ya mashamba.

“Kuna njia ya kufuatilia haki katika serikali yetu bila kuchukua sheria mkononi,” akasema.

mongala@ke.nationmedia.com

  • Tags

You can share this post!

NDIVYO SIVYO: Ni kosa kusema ‘gwara’, unafaa kusema...

Namwamba aahidi kufufua sekta ya michezo nchini

T L