Habari Mseto

Naibu chifu alinitandika bila sababu, asema ajuza

May 15th, 2018 1 min read

Na VIVIAN JEBET

AJUZA wa miaka 68 anadai kushambuliwa na naibu wa chifu mjini Isiolo bila kufanya kosa, alipokuwa ameenda kumchukua mwanawe kwenye makazi ya mshukiwa.

Kamishna wa kaunti hiyo, Bw Mwachaunga Chaunga alisema hajapata habari za kushambuliwa kwa Bi Kana Galgalo, lakini akawaonya machifu na manaibu wao dhidi ya kudhulumu raia.

“Akipatikana na hatia, naibu chifu huyo atachukuliwa hatua,” akasema.

Bi Galgalo, aliyeripoti kisa hicho katika Kituo cha polisi cha Isiolo, alidai kuwa naibu huyo wa chifu amesababisha wakazi wengi kutotafuta huduma muhimu za serikali.

Alisema kwamba hawawezi kuripoti masuala ya usalama, kwa hofu za kudhulumiwa.