Naibu Gavana ahofia ODM kupoteza ugavana Kaunti ya Kilifi

Naibu Gavana ahofia ODM kupoteza ugavana Kaunti ya Kilifi

NA ALEX KALAMA

NAIBU Gavana wa Kaunti ya Kilifi, Bw Gideon Saburi, ameeleza wasiwasi kwamba huenda Chama cha ODM kikakosa kushinda kiti cha ugavana wa kaunti hiyo kwenye uchaguzi ujao.

Kulingana naye, kuchelewa kwa mgombeaji ugavana wa ODM, Bw Gideon Mung’aro, kuchagua mgombea mwenza kunazidi kuathiri kampeni zake.

“Tukiwa tutakuwa bado tunavutana miguu wale wengine wako mbioni. Saa hizi sisi bado tunafikiria naibu atakuwa nani. Tunataka sasa tuamue ili tuingie katika kampeni,” alisema Bw Saburi.

Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita, Bw Saburi alisema wanachama wa ODM nyanjani wanashindwa kuvumisha chama kwa vile hakuna mwelekeo halisi kutoka kwa wale wanaotarajiwa kuongoza chama katika kaunti.

“Tuwawezeshe wale ambao tutawapatia mamlaka ya kule nyanjani ili watafute hizi kura, kwa sababu kura hazitapatikana tukiwa tunakaa kwenye vikao vya ukumbini. Lazima tutoke tukazitafute kuhakikishe tunajaza kapu. Na kapu la kwanza ambalo ni tuhakikishe limejaa ni la Raila Odinga hilo kapu hilo lazima tulijaze,” akasema Bw Saburi.

Bw Saburi ni mmoja wa waliotajwa kuzingatiwa kuwa mgombea mwenza wa Bw Mung’aro, ambaye kufikia Jumatatu alikuwa hajatangaza mgombea mwenza wake.

You can share this post!

Pigo KPA ikipoteza ardhi ya mamilioni

Mutua, Kingi watafuta hifadhi kwa Ruto, wadai kuumizwa...

T L