Naibu Rais akutana na Raila

Naibu Rais akutana na Raila

NA SAMMY WAWERU

NAIBU Rais Rigathi Gachagua amekutana na kinara wa Azimio, Raila Odinga.

Leo Ijumaa, Bw Gachagua amepakia picha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook akiwa na Bw Odinga aliyeibuka wa pili kwenye uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022.

“Tuna heshima kwa raia wetu wakuu. Nimeridhia asubuhi ya leo kukutana na aliyekuwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Raila Odinga Mombasa,” chapisho la Naibu Rais limeeleza.

Wawili wao wamefanya mkutano huo katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege, Mombasa.

Bw Gachagua jana alizindua kongamano la mafunzo ya magavana waliochaguliwa Agosti 9, 2022, linaloendelea mjini Mombasa.

Kongamano hilo la siku tatu, hasa linanuwia kufunza magavana wapya utendakazi.

Rais William Ruto anatarajiwa kuhutubia magavana kesho Jumamosi wakati likikunja jamvi.

Bw Raila alimenyana na Dkt Ruto kuwania urais katika uchaguzi mkuu uliokamilika, kesi yake kupinga matokeo ya kura za urais katika mahakama ya upeo ikifutiliwa mbali na korti.

Akizungumza baada ya uapisho wa Gavana wa Mombasa jana Alhamisi, Bw Abdulswamad Nassir, kiongozi huyo wa ODM alishutumu idara ya mahakama kwa uamuzi iliyotoa.

  • Tags

You can share this post!

Wakenya waambiwa wawe tayari kuumia

Vidokezo muhimu kupunguza uharibifu wa chakula

T L