Nairobi, kaunti za Mlima Kenya zaorodheshwa tajiri zaidi Kenya

Nairobi, kaunti za Mlima Kenya zaorodheshwa tajiri zaidi Kenya

Na CHARLES WASONGA

KWA mara nyingine Nairobi na kaunti za Mlima Kenya zimeorodheshwa kama tajiri zaidi kulingana na takwimu zilizotolewa na Shirika la Kitaifa la Takwimu Nchini (KNBS).

Kulingana na makadirio yaliyotolewa na shirika hilo Jumatatu, Nairobi ina kiwango cha chini zaidi cha umaskini cha asilimia 16.8 ikifuatwa na Nyeri na Meru zenye kiwango cha umaskini cha asilimia 19.

Kaunti za Kirinyaga na Kiambu zina kiwango cha umaskini asilimia 22 na 23, mtawalia.

Narok na Machakos nazo ziliandikisha viwango vha umaskini vya asilimia 23, kila moja huku Muranga, Tharaka Nithi na Mombasa zikifunga orodha ya kaunti tajiri kwa kuwa na viwango vya umaskini vya asilimia 25, 24, na 27.

Kaunti ya Turkana nayo inaongoza katika orodha ya kaunti maskini zaidi nchini.

Kaunti hiyo iliyoko eneo kame la kaskazini mwa Kenya ina kiwango cha umaskini cha asilimia 79.4. Hii ina maana kuwa familia nyingi haziwezi kumudu gharama ya mahitaji ya kimsingi kama vile chakula, nyumba, maji safi, huduma za afya na elimu.

Kaunti nyinginezo zenye kiwango kikubwa cha umaskini ni Mandera, Samburu, Busia na Garissa.

Nyingine ni Marsabit, Wajir, Tana River, Pokot Magharibi na Isiolo zenye viwango vya umaskini vya asilimia 63.7, 62.6, 62.2, 57.4 na 51.9, mtawalia.

Kulingana na KNBS familia zenye mapato ya Sh3,252 kwa mwezi katika maeneo ya mashamba na zile zinazopata Sh5,995 kila mwezi zinaishi katika miji mikuu nchini.

Ripoti hiyo hata hivyo, inaonyesha kuwa kaunti 35 kati ya 47 zimeandisha viwango vya kuimarika kwa hali ya maisha tangu 2013, ugatuzi ulipoanza kutekelezwa.

Kwa upande mwingine ni kaunti 12 pekee ambazo hazijaandikisha kuimarika kwa viwango vya ubora wa maisha.

You can share this post!

Wanawake watwaa majukumu ya kiume wazee wakilewa tu!

Barcelona wamtia Messi kwenye orodha ya masogora...