Nairobi kunoma, asimulia rapa Majirani

Nairobi kunoma, asimulia rapa Majirani

NA TOM MATIKO

UNAMKUMBUKA rapa Majirani aliyetoka nyuma kidogo na hiti kama Tukumbukeko na Hivyo Ndio Kunaendaga?? Majirani kaamua kurudi vijijini baada ya maisha ya mjini Nairobi kuwa magumu kwake.?

Kipindi akitoka, alikuwa kasainiwa kwenye lebo ya Grand Pa iliyokuwa ikimilikiwa na produsa Reffigah.

Lakini baada ya lebo hiyo kupoteza mwelekeo na kupotea kwenye gemu, wasanii kibao mastaa waliokuwa wamesainiwa pale nao walizama akiwemo Majirani ambaye hajasikika kwa muda kisanii.?Juzi kati kuliibuka video ambayo anaonekana akipasua mawe ya ujenzi.

Baada ya video hiyo kuzagaa, tulijitahidi kumsaka na kauli yake ni kwamba maisha ya mjini Nai, yalimlemea.

“Nilikuja Nairobi kusaka maisha ila baada ya menejimenti kusambaratika, nilisaka nyumba nikaanza kulipia. Nilihangaika kupata kazi na mwishowe nikafungiwa nyumba kwa sababu ya ukosefu wa kodi. Baadaye video yangu nikifanya kibarua cha kupasua mawe kwenye kware ikasambaa na kila mtu akanicheka. Sasa nimeamua kuachana na muziki nirudi kijijini nianze upya, nimechoka kuishi maisha feki,” Majirani kakata kauli.

You can share this post!

WANDERI KAMAU: Jamii imefeli ila ijikakamue kuelekeza...

Tapeli mkubwa wa Showbiz Wilkins Fadhili acheza kama yeye...