Habari Mseto

Nairobi yaanza kupungukiwa na pato baada ya kupunguza ada ya uegeshaji

January 23rd, 2019 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Licha ya kupunguza ada ya kuegesha magari hadi Sh200 kwa siku, serikali ya Kaunti ya Nairobi inapoteza Sh300, 000 kwa siku.

Kwa siku, kaunti hiyo ilikuwa ikikusanya Sh1.5 milioni lakini hivi sasa inakusanya Sh1.2 milioni baada ya mwanzo wa utekelezaji wa agizo jipya mapema mwaka huu.

Ripoti hii ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa huduma za uegeshaji wa Nairobi Bw Tom Tinenga.

Licha ya upungufu huo, idadi ya magari ya kibinafsi imeongezeka kutoka 4,500 hadi 5,200 kwa siku.

Awali, ada ya kuegesha ilikuwa ni Sh300 kwa siku kabla ya kupunguzwa mnamo Januari 14.

Bw Tinega alitetea hatua ya serikali ya kaunti kwa kusema serikali hiyo imejitolea kuwahudumia wakazi wa Nairobi ila haipo kupata faida.